HUKU kukiwa na madai kwamba mwigizaji Kajala Masanja ana uhusiano wa ‘kikubwa’ na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, mwigizaji huyo amezidi kuyachochea moto madai hayo kwa kutokana na kujiachia mara kwa mara na dada wa Diamond, Queen Darleen, Risasi Mchanganyiko linakujuza. Kwa mujibu wa chanzo makini, Kajala na Queen Darleen wamekuwa ‘beneti’ kila kona ambapo pia kuna fununu kuwa hata familia ya Diamond imebariki uhusiano wake na Mbongo Fleva huyo na wanampa ushirikiano wa kutosha Kajala. Mwishoni mwa wiki hii, paparazi wa GPL aliwanasa laivu Kajala na Queen Darleen katika fukwe za White Sands, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam walipokuwa wameenda kupunga upepo na kuwapeleka watoto wao kuogelea. Kuonekana kwa wawili hao kuliibua gumzo la aina yake ambapo wafuatiliaji wa ‘ubuyu’ walionekana kunong’onezana kuwa yale waliyokuwa wakiyasikia na kuyasoma kwenye mitandao kuwa Kajala ana uhusiano na Diamond, yana ukweli. “ Itakuwa ni kweli Diamond anam...
asante ndeti
ReplyDelete