Posts

Showing posts with the label Michezo

Haya Hapa Matokeo ya Mechi ya Simba na Prison ya Mbeya Iliyochezwa Leo Jioni.....

Image
Wakati watani zao wa jadi Yanga wamemaliza kucheza mchezo wao wa kwanza wa raundi ya pili katika michuano ya klabu bingwa Afrika dhidi ya APR ya Rwanda kwa ushindi wa goli 2-1 March 12, Simba wao wameshuka dimbani March 13 kuendeleza harakati zao za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara. Simba wameshuka dimbani kucheza dhidi ya klabu ya wajelajela wa Mbeya Tanzania Prisons, katika mchezo wao 23 wa Ligi Kuu Tanzania bara. Simba waliingia uwanjani kuhakikisha wanapata point tatu ili waendelee kuwa katika nafasi nzuri ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara. Hata hivyo licha ya jitihada kubwa kuoneshwa ndani ya dimba la uwanja wa Taifa na Tanzania Prisons za kuataka kutoa sare, hazikuzaa matunda, kwani Simba ilifanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 kupitia kwa Awadh Juma dakika ya 88. Kwa matokeo hayo Simba anaendelea kuongoza Ligi akiwa na jumla ya point 54 akifutiwa na Yanga aliyemzidi point 3 na michezo miwili.

Photos from LeBron James' final duel with rival Kobe Bryant last night

Image
Kobe Bryant and Lebron James, the Lionel Messi and Cristiano Ronaldo of Basket ball, battled for the last time last night at the Staples center and it was an emotional as well as magical night. LeBron James sent out an emotional tribute to Bryant before tip-off. "Best of luck with your new journey after you leave this beautiful game behind," James wrote on Bleacher Report's Uninterrupted. "I'll do my part to grow it, to make it as great as you made it and leave it for the next group that comes behind me and the rest of the guys." Kobe Bryant scored 26 points compared to Lebon's 24 as the retiring Kobe still showed he was the better player despite his imminent retirement.

Cristiano Ronaldo is labelled 'Spornosexual' by Mark Simpson who authored the term 'metrosexual'

Image
According to Mark Simpson who created the term 'metrosexual', (which refers to a straight man who embraces the homosexual lifestyle, i.e. refined tastes in clothing, excessive use of designer hygiene products, a straight guy who’s so cool, smart, attractive, stylish, and cultured, that everyone thinks he’s gay), football star Cristiano Ronaldo is a Spornosexual. Ronaldo has always been seen as the classic metrosexual: grooming and taking care of his appearance with meticulous care, and always sporting the latest fashion trend. Speaking in an interview with Catalan paper La Vanguardia yesterday, Simpson labeled Cristiano Ronaldo as a classic ‘Spornosexual‘implying he was at the forefront of the new frontier of men. "(Spornosexual is) a fusion of sport and porn: cultivating an athletic body as an object of desire, and showing it off on social networks, accumulating sexual partners.' 'It’s a tendency with young men. Look at Cristiano Ronaldo:...

Choma Gari Sasa :Haya Ndio Matokeo ya Mechi Aliyohaidi Madee Kuchoma Gari yake Moto Kama Arsenal itafungwa

Image
Jumapili ya January 24 Ligi Kuu Uingereza iliendelea kwa michezo miwili kupigwa, mchezo wa kwanza kuchezwa ulikuwa mchezo kati ya Everton dhidi ya Swansea City mchezo ambao ulimalizika kwa Swansea kuibuka na ushindi wa goli 2-1 licha ya kuwa katika uwanja wa ugenini. Mchezo wa pili ulikuwa ndio mchezo ulioteka hisia za watu wengi zaidi wa jiji la London, kwani ulikuwa unazikutanisha timu za jiji moja Arsenal dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Emirates, hisia za mchezo huo hazikuishia Ulaya pekee, Tanzania msanii wa Bongo Fleva Madee Ali alitangaza kuwa kama endapo Chelsea itaifunga Arsenal basi atachoma moja kati ya magari yake moto, Kwa bahati mbaya licha ya kuwaArsenal walikuwa na mwenendo mzuri katika Ligi msimu zaidi ya Chelsea, walikubali kipigo cha goli 1-0 kutoka Chelsea wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani. Goli la Chelsea lilifungwa na Diego Costa dakika ya 23, goli hilo lilipelekea Madee kutopatikana hewani. Kwa matokeo hayo Chelsea wanatimiza point 28 n...

Sakata la Katibu wa Yanga Kuondoka Yanga..Manji Afunguka Mazito

Image
TAARIFA KWA WANAYANGA KUPITIA VYOMBO YA HABARI 1. Baada ya kuupitia uamuzi wa Kamati ya Nidhamu kuamua sababu kuvunja mkataba kati ya klabu Yanga na mchezaji Haruna Niyonzima, nilihisi kulikuwa kuna kasoro hasa kwa mchezaji anayelipwa mshahara wa Sh milioni 6 anaweza vipi kupuuzia maisha yake na kuanzisha mgogoro usiokuwa na tija kwa maisha ya kipato. (angalia kiambatanisho 1) Niliamua uchunguzi wa ndani ufanyike katika suala hilo zima na mwisho, Jonas Tiboroha alibainika kuwa hakuwasilisha ushahidi ya mawasiliano sahihi kwa Kamati ya Nidhamu kuhusiana na Haruna Niyonzima, hali iliyosababisha kamati kuchukua uamuzi ambao haukuwa sahihi kwa sababu; Kulifanyika mambo ambayo hayakuwa sahihi, mfano barua za Niyonzima kutoka kwa Shirikisho la Soka la Rwanda (Ferwafa) ambazo zilitumwa kwa TFF na kupokelewa kama ambavyo Azam FC walipokea ya mchezaji wao kupitia kwa Afisa Mtendaji Mkuu wao. Lakini barua ya Niyonzima kuja Yanga, ilionekana haikupokelewa kama ilivyokuwa k...

MAKUBWA..Mwanamuziki wa Bongo Kuchoma Gari lake Moto Endapo Arsenal itafugwa na Chelsea leo

Image
Leo kutakuwa na mchezo mkali wa ligi kuu ya England kati ya mabingwa watetezi Chelsea dhidi ya Barcelona. Msanii Madee ni mmoja wa mashabiki wa Arsenal ambaye leo atakuwa mpinzani mkubwa wa Chelsea. Katika kuonyesha mapenzi yake kwa klabu yake ya Arsenal, kwenye ukurasa wake wa @Instagram Madee ameahidi kuchoma gari yake moja moto endapo timu yake ya Arsenal itafungwa na Chelsea. Hivi ndivyo alivyoandika.. "Tukifungwa leo na chelsea nachoma gari yangu moja moto" Madee

MBWANA SAMATTA AMTEMBELEA WAZIRI NAPE OFISINI KWAKE.

Image
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta leo amekutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Mh. Nape Nnauye kwenye ofisi ya Waziri huyo kwa ajili ya kumuaga kwa niaba ya serikali kabla ya kuelekea nchini Nigeria kuhudhuria sherehe za ugawaji wa tuzo za wachezaji bora wa Afrika. Samatta amesema anatambua umuhimu wa mchango wa serikali katika kuchangia mafanikio yake pamoja na soka la Tanzania kwa ujumla na kuongeza kuwa, endapo atafanikiwa kutwaa tuzo hiyo basi haitakuwa ya kwake binafsi bali ni ya taifa zima. “Kama nitafanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika tuzo hiyo haitakuwa ya kwangu peke yangu bali itakuwa ni ya watanzania wote pamoja na Tanzania kama nchi”, amesema Samatta ambaye yupo kwenye orodha ya wachezaji watu ambao wameingia fainali ya kuwania tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa wachezaji wa ligi za Afrika. “Kabla ya kwenda sehemu yoyote ile ni lazima upate baraka za wazee ndiyomaana nimekuja hapa kuaga ...

JE KUMTIMUA MOURINHO NI MAAMUZI SAHIHI KWA MUSTAKABALI WA CHELSEA? KITENDO WALICHOKIFANYA WACHEZAJI WA CHELSEA NI CHA KIPUUZI

Image
Mashabiki wengi wa Chelsea wamefuraishwa sana na matokeo ya mechi ya Jana kati ya Chelsea na Sunderland baaada ya kuibuka na ushindi wa mabao matatu kwa moja Lakini tujiulize kuhusu mustakabali wa Chelsea miaka mitano au kumi ijayo Je kumtimua Mourinho ni maamuzi sahihi kwa mustakabali wa Chelsea? Mimi naona sio sahihi kuendekeza sana wachezaji wa chelsea kuamua boss wao awe nani.La sivyo baada ya miaka kumi tusishangae Chelsea ikiwa imefundishwa na walimu zaidi ya 20   na hakipaswi kushabikiwa na wote waipendao Chelsea  Wamehujumu timu na sio Mwalimu.. Leo Mourinho yuko wapi? Na timu ipo nafasi ngapi? Walichokifanya Wachezaji ni Usaliti na Uhujumu ni bora kuwa na wachezaji wabovu wenye nidhamu kuliko hao would Class prayers wasio na nadhimu na timu Shame Hazard,Shame Costa and you're thinking to be the world prayer

NAPE: NITAANZA KUSHUGHULIKIA SHERIA NA NIDHAMU MICHEZONI

Image
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye ameahidi kushughulikia sheria mbalimbali zinazosimamia sekta hiyo ili kuongeza nidhamu michezoni. Nape aliyeapishwa juzi kuanza kibarua hicho, ataiongoza wizara hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Dk Fenella Mukangara, huku ndoto za Watanzania zikiwa ni kuona kiwango cha michezo kilichoporomoka, kinakua. Akizungumza na mwandishi wetu jana alisema utovu wa nidhamu kwa baadhi ya viongozi na wachezaji umekuwa ukiitafuna sekta hiyo kwa kiwango kikubwa na kusababisha kushuka kwa michezo. Alisema zipo baadhi ya sheria zinazohitaji marekebisho ili ziwe na tija na kwamba ana uhakika kuwa zitasaidia kurejesha thamani ya michezo, ikiwamo soka na sanaa. “Michezo ikisonga mbele na timu zetu zikifanya vizuri tutavutia wawekezaji wengi kwenye sekta hii kwa sababu suala siyo kufurahi, tunatakiwa tuichukulie sekta hii muhimu kama sehemu ya kuzalisha ajira na kukuza uchumi wa Taifa letu na mtu binafsi,” ...

HAWA NDIYO WANAUME 9 WALIOPIGA HAT-TRICK NDANI YA EPL HADI SASA, WA-AFRIKA WAWILI NDANI

Image
Mwezi November ulikuwa ni mgumu kwa timu nyingi za EPL. Hat-trick moja tu ulifungwa ndani ya mwezi huo na hiyo inaashiria ni kwa kiasi gani timu zilipambana kusaka goli. Lakini mshambuliaji wa Everton Arouna Kone ndiye mchezaji pekee aliyefunga hat-trick ndani ya mwezi huo. Hii ni orodha ya wachezaji tisa ambao wamefanikiwa kufunga hat-trick ndani ya EPL msimu huu hadi sasa huku orodha hiyo ikijumuisha wachezaji wawili kuoka bara la Afrika. 9. Callum Wilson-Bournemouth Ilikuwa ni August 22, 2015 mechi kati ya West Ham dhidi ya Bournemouth. Cullum Wilson aliweza kufunga hat-trick yake, alifunga goli mbili kwenye kipindi cha kwanza (dakika ya 11 na 28) kisha akaikamilisha kwa mkwaju wa penati dakika ya 79 na kuipa ushindi timu yake ushindi wa magoli 4-3. 8. Steven Naismith-Everton September 12, 2015 Everton ilicheza dhidi ya Chelsea, siku hii ilikuwa ni nzuri kwa Steven Naismith baada ya kufanikiwa kurudi kambani mara tatu dakika ya 17, 22 na ...

KAMATI SAIDIA STARS NA TFF WASUTANA NA KUONYOOSHEA VIDOLE MCHANA KWEUPE....

Image
Kamati ya Saida Taifa Stars ishinde imemaliza kazi na kuvunjwa rasmi jana, lakini nyuma yake imeacha maswali mengi kuliko majibu kuhusu utendaji na uhusiano wake na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Rais wa TFF, Jamal Malinzi aliunda kamati hiyo ili kuhamasisha Stars iishinde Algeria na kufuzu hatua ya makundi kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia mwaka 2018, badala yake Stars ikaishia kufungwa jumla ya mabao 9-2. Jambo kubwa lililozua mkanganyiko ni suala la usafiri wa ndege kwa ajili ya Stars kwenda Algeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano. Awali, kamati hiyo chini ya Mwenyekiti Farough Baghozah, ilidai kupata udhamini kutoka kwa Kampuni ya Fastjet waliotoa punguzo la gharama za tiketi kwa wachezaji kufikia dola 700 (Sh. Milioni 1.4) kwenda na kurudi kwa mtu mmoja. Hata hivyo, wakati kamati hiyo ikiandaa mipango ya usafiri kupitia Fastjet, TFF ikaja na mipango yake na kuamua kutumia ndege ya Uturuki (Turkish Airways) kwa gharama ya dola 1,200 (Sh....

TIMU YA TAIFA YA VIJANA WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 15 U15 YAINGIA KAMBINI

Image
  Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15) imeingia kambini jana jioni katika hosteli za TFF zilizopo Karume jijini Dar es salaam, kujiandaa na ziara ya mafunzo katika ukanda wa Afrika Mashariki itakayoanza Disemba Mosi mwaka huu.