Posts

Showing posts with the label Education

Updates za Habari ya Kufutwa Kazi Kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo na Wenzake..Walioteuliwa Kushika Nafasi Hizo Hawa Hapa

Image
Waziri wa Elimu Sayansi, Teknolojia na ufundi, Prof Joyce Ndalichako amesitisha mkataba wa kazi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo George Nyatenga (Pichani chini). Pia amewasimamisha kazi Wakurugezi watatu wa Bodi hiyo ambao ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Yusufu Kisare, Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo Juma Chagonja na Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo. Prof. Ndalichako amemwagiza Mkaguzi wa ndani Mkuu wa Serikali ahakiki maelezo na Nyaraka zilizowasiliwa na Bodi ya Mikopo pamoja na kufanya ukaguzi maalum kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2013 hadi sasa. Amewateua wafuatao ku Kaimu nafasi; Kaimu Mkurugenzi Mtendaji mteule ni Bw. Jerry Sabi kutoka Mzumbe University na Kaimu Mhasibu Mkuu mteule ni Bw. Daniel Mafie kutoka NECTA

23rd November 2015 12:37:24 TANGAZO KWA UMMA - UENDESHAJI WA KOZI YA STASHAHADA (DIPLOMA) YA MENEJIMENTI NA UALIMU KATIKA CHUO KIKUU CHA ECKERNFORDE – TANGA

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE) TANGAZO KWA UMMA UENDESHAJI WA KOZI YA STASHAHADA (DIPLOMA) YA MENEJIMENTI NA UALIMU KATIKA CHUO KIKUU CHA ECKERNFORDE – TANGA Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) lina utaarifu umma kuwa Stashahada (Dilploma) ya Menejimenti na Ualimu itolewayo katika Chuo kikuu cha Eckernforde - Tanga ilipata ithibati ya Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) na kuruhusiwa kutolewa katika kampasi yake ya Tanga. Hata hivyo imefahamika baadae kuwa chuo hicho kimekuwa kikitoa mafunzo hayo katika kampasi zisizoruhusiwa ikiwamo vituo vya shule za msingi kwenye wilaya mbalimbali nchini. Tume ya Vyuo vikuu ilishatoa katazo la maandishi kwa Eckernforde na kwenye vyombo vya habari lakini bado fomu za kujiunga na programu hiyo zimekuwa zikiendelea kugawiwa katika vituo mbalimbali nchini.