Posts

Showing posts with the label News

Watupwa Jela Miaka 60 Kwa Kukutwa Ngozi za Chui na Chatu

Image
Mahakama ya Mkoa wa Manyara imewahukumu watu watatu kifungo cha miaka 60 jela kwa kosa la kukutwa na nyara za Serikali, ikiwamo ngozi ya chui na nyoka aina ya chatu. Washtakiwa hao ni Mathayo Mchono, Bura Massay, wakazi wa Gembaku wilayani Mbulu na Bryson Jacob wa Bashey wilayani Karatu. Hakimu Bernad Nganga amesema leo kuwa mahakama hiyo imetoa hukumu hiyo baada ya ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka kuwatia hatiani washtakiwa hao. Hakimu Nganga amesema kila mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka 20 gerezani. Awali, waendesha mashtaka, Linus Bugaba na wakili wa Serikali, Timotheo Mmari waliiomba mahakama itoe adhabu kali iwe fundisho kwa wengine. Ilidaiwa kuwa washtakiwa hao walikamatwa Novemba 30, 2014 eneo la Kilima Punda wilayani Mbulu wakiwa na ngozi ya chui yenye thamani ya Sh6.3 milioni na ya chatu ya Sh648,000.   

Ukiendelea Na Tabia Hizi Mafanikio Kwako Yatakuwa Ni Ndoto....

Image
Hasira za mafanikio zinatofautiana baina ya mtu mmoja na mwingine. Kama kweli unahitaji mafanikio ya kweli ni lazima uwe na hasira ya njaa kama aliyonayo simba. Miongoni mwetu ni watu wachache sana wanatambua hasira hii ya mafanikio, wengi wetu huchukulia mafanikio kwa sura ya kawaida sana na mwisho wa siku tunaishia kuwa maskini. Binadamu ni kiumbe wa ajabu sana, nasema hivi ni kiwa na maana ya kwamba binadamu anapenda sana maisha ya kufanyiwa kila kitu, kwa mfano mtu anapenda umpikie chai, umuwekee kwenye chupa, umuwekee chai kwenye kikombe na umgorogee  na sukari katika chai na ukishamfanyia yote hayo subiri anywe hiyo chai uone atakavoanza kulaamu utamskia anasema sukari imezidi au sukari hajikolea na lawama zingine nyingi,  kitu cha kujiuliza je, mtu huyo alishindwa kuweka sukari mwenyewe kwenye chai yake ili jambo lolote likitokea akose wa kumlamu. Mtu huyo huyo ukimuuliza unafanya biashara gani? Utamsikia anasema sifanyi biashara y...

Watu 42 Watiwa Mbaroni Zanzibar Wakituhumiwa Kulipua Nyumba ya Kamishna wa Polisi

Image
Jeshi la Polisi Zanzibar linawashikilia watu 42 wakituhumiwa kuhusika na mlipuko uliotokea juzi usiku katika nyumba ya Kamishna wa Polisi, Hamdan Omar Makame. Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya polisi Ziwani, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam alisema hadi jana mchana watu 42 walikuwa ndani kwa ajili ya kuhojiwa na jeshi hilo. Alisema uchunguzi unaendelea na bado watu wengine wanatafutwa kuhusiana na tukio hilo. “Bado tunaendelea na uchunguzi wa jambo hili na tukishakamilisha tutatoa taarifa rasmi,” alisema Kamanda Mkadam.

Video:Bob Junior Kakubali Alikamatwa na Kulala Polisi.. Chanzo Je? Stori Iko Hapa

Image
Ni headlines zilizochukua nafasi kubwa katika mitandao mbalimbali  hivi karibuni kuhusiana na msanii Bob Junior kukamatwa na jeshi la polisi, sasa basi msanii huyo yuko uraiani na hapa amefunguka mengi ambayo tulikuwa hatuyafahamu kuhusu kukamatwa kwake. Angalia Video Hapa: Chanzo:Millard Ayo

Kesi ya IPTL Dhidi ya Zitto Kabwe kusuluhishwa Machi 23 Kwa Siri

Image
Mahakama Kuu inatarajia kusuluhisha kesi iliyofunguliwa na Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) dhidi ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe na wenzake Machi 23, mwaka huu. Kesi hiyo namba 175 ya mwaka 2014 ilipangiwa kuanza kufanyiwa usuluhishi jana mbele ya Jaji Salvatory Bongole, lakini ilishindikana kutokana na upande wa walalamikaji ambao ni IPTL kushindwa kufika mahakamani. Hata hivyo, Kaimu Msajili wa Mahakama hiyo Kitengo cha Usuluhishi, Beda Nyaki alisema kesi hiyo itasikilizwa kwa siri baina ya pande hizo. “Kesi hii haiwezi kuripotiwa kwenye vyombo vya habari kwa sababu ipo katika hatua za kwanza za usuluhishi, hivyo kitu kitakachoongolewa baina ya walalamikaji na walalamikiwa kitakuwa ni siri yao,” alieleza Nyaki. Alisema kusikilizwa kwa faragha kwa kesi hiyo ni hatua ya kupunguza gharama na muda. Katika kesi hiyo, Kampuni za IPTL, Pan Africa Power Solutions (T) Limited na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni...

MACHANGUDOA 287 Dar es Salaam Wakiona Cha Moto...Wakamatwa Pomoja na Wateja Wao na Kuswekwa Polisi

Image
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kuwakamata jumla ya watu 287 ambao ni dada poa pamoja na kaka poa katika operation maalum iliyofanyika maneo mbalimbali ya Jiji hilo. Operation hiyo ilitangazwa na kamishna wa kanda maalum mnamo Tarehe 7 mwezi wa 3 na kuazimia kuwakamata madada poa na makaka poa pamoja na wateja wao ambao watakutwa wakiwanunua. Katika mkoa wa kipolisi wa ilala operation hii imefanikiwa kuwakamata jumla ya madada poa 51 kutoka katika maeneo mbalimbali yakiwemo msimbazi,Buguruni,na stakishari,pia imewakamata jumla ya makaka poa 12 ambapo 11 wanatokea Buguruni na mmoja kutoka msimbazi. Mkoa wa kipolisi wa temeke umefanikiwa kuwakamata jumla ya madada poa 22,ambapo changombe walipatikana 12,na mbagala walipatikana madada poa 10. Aidha katika mkoa wa kipolisi wa kinondoni operation hiyo imefanikiwa kuwakamata madada poa 76 kutoka maeneo ya osyterbay madada poa 49,magomeni 23,na kawe madada poa 4,pamoja na makaka poa...

VIDEO: EXCLUSIVE: Paul Makonda Kaongea nini Baada ya Kupewa Ukuu wa Mkoa Dar?

Image
Headline zilizoongoza kwenye magazeti ya Tanzania March 14 2016 ni kuhusu uteuzi wa wakuu wa mikoa nchini, miongoni mwa waliozikamata zaidi headline hizo ni aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda. Sasa baada ya hayo yote, Paul Makonda akatangazwa kwamba ndio Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es salaam, wakati akitangazwa hakuwa akijua kwamba atatangazwa kuwa Mkuu wa Mkoa. ‘Leo nilikuwa natimiza mwaka mmoja tangu kuteuliwa kwangu kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, pia nilienda kuzindua  na kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa jengo laupasuaji katika hospitali ya Mwananyamala‘ Alizipata vipi taarifa za kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa? ‘Sina uhakika zaidi kwasababu mtu hata akipiga simu mimi nilikuwa najua ni utani, lakini nilikuja kuamini baada ya kuliona jina langu kwenye karatasi yenye nembo ya Serikali ‘ ;- Paul Makonda

AJALI: Basi la Leina Tours lapata ajali Kimara Bucha

Image
Basi la Leina Tours lililokuwa likitokea Kahama kuja Dar es Salaam, limeacha njia na kutumbukia katika mtaro eneo la Kimara Bucha  usiku  wa kuamkia leo Idadi ya waliofariki haijafahamika  ila waliojeruhiwa ni zaidi ya 30 na walikimbizwa  Haospitali  ya  Mwananyamala na Muhimbili.

Wafanyakazi Waliofukuzwa NIDA Wagoma Kupokea Barua Za Kuachishwa Kazi

Image
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) waliofutiwa mikataba ya kazi, wamegoma kupokea barua za kuachishwa kazi wakidai kwamba hawajui kilichoandikwa kuhusu hatima ya madai yao. Wafanyakazi hao walikutana jana Dar es Salaam na kiongozi wao, Seif Kibangu alisema wamekubaliana kutochukua barua hizo hadi pale watakapopata ushauri kutoka kwa wanasheria. “Licha ya mishahara ya miezi mitatu tuna madai yetu mengine ikiwamo makato ya mafao yetu yaliyotakiwa kupelekwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, pia tumekuwa tukikatwa bima ya afya asilimia tatu ya mishahara yetu hatujui hatma yake.  "Sasa leo wanataka tuchukue barua hizo tena kwa kusaini kabla ya kujua kilichoandikwa hapana tuendelee kuvumilia haki yetu tutaipata,” alisema Kibangu. Aliwakosoa waliochukua barua hizo akisema waliajiriwa kwa makundi, ingawa pia wapo waliopewa kazi hiyo kwa vimemo. “Hili ni jasho letu, hatuibi cha mtu kwa hiyo tunastahili kupata h...

Mwenyekiti wa CHADEMA Ahukumiwa Kifungo cha Miezi 6 Kwa Kosa la Kumsaidia Ndugu Yake Kujitetea Mahakamani

Image
Mwenyekiti wa Chadema, Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, Jacob Munyaga (60), amehukumiwa adhabu ya kifungo cha miezi sita gerezani kwa kosa la kumsaidia ndugu yake maelekezo ya namna ya kujitetea mahakamani. Ilidaiwa kuwa kiongozi huyo alimsaidia mtuhumiwa Charles Mloba namna ya kujieleza mahakamani dhidi ya shauri la kujeruhi linalomkabili, kinyume cha sheria inayotoa fursa hiyo kwa mawakili pekee. Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya hiyo, Francis Kishenyi akitumia kifungu cha 114(1) (A) cha Sheria ya Makosa ya Jinai namba 16 ya mwaka 2002 inayotoa adhabu kwa yeyote anayefanya kazi ya uwakili au usaidizi wa kisheria bila kuwa na sifa. “Kwa mujibu wa kifungu hicho, adhabu kwa mshtakiwa inaweza kuwa kulipa faini ya Sh500 au kifungo cha miezi sita jela. "Mahakama hii imeamua utumikie kifungo cha miezi sita jela kwa sababu umebainika kufanya vitendo hivi mara kwa mara,” alisema hakimu huyo. Alisema mshtakiwa huyo ana haki ya kukata...

Mwanafunzi Auawa Kwa Ugomvi wa Chaja ya Simu....

Image
Watu wawili wamefariki dunia mkoani Dodoma katika matukio mawili tofauti likiwemo la mwanafunzi wa chuo cha serikali za mitaa Hombolo, Basil Msabila (24) kuuawa kwa kupigwa na chuma kichwani na mwenzake aitwaye Charles Makele (19) kwenye ugomvi wa kugombea chaja ya simu. Akizungumza na waandishi wa habari, kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa amesema kuwa tukio hilo lilitokea Machi 6 mwaka huu katika chuo cha serikali za mitaa kilichopo Hombolo katika Manispaa ya Dodoma. Amesema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kugombania chaja ya simu ambayo ni mali ya marehemu katika chumba cha bweni ambapo wanaishi wanafunzi wanne. Katika tukio la pili mtu mmoja mwanaume ambaye hakufahamika jina lake mara moja aliuawa na watu wenye hasira katika eneo la kisasa lililopo katika Manispaa ya Dodoma baada ya kukutwa akivunja dirisha la mtu. Aidha ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma kutojichukulia sheria mkononi na ...

Marekani Yatia Mguu Tanzania....Yataifisha Mali za Mtanzania Kigogo wa Madawa Ya Kulevya

Image
Serikali ya Marekani imeamua kutaifisha mali za mfanyabiashara wa dawa zilizopigwa marufuku za kulevya kutoka Tanzania, Ali Khatib Haji Hassan, maarufu kwa jina la “Shikuba” na mtandao wake na kupiga marufuku kampuni za nchi hiyo kujihusisha na biashara zake. Shikuba, ambaye amekuwa akihusishwa na biashara kubwa ya usafirishaji dawa za kulevya kati ya Afrika Mashariki, Asia, Ulaya na Marekani, alikamatwa mwaka 2014 nchini Tanzania akihusishwa na shehena ya kilo 210 za heroin zilizokamatwa mkoani Lindi mwaka 2012. Taarifa iliyotolewa juzi na kitengo cha udhibiti wa mali za nje cha Wizara ya Fedha ya Marekani imeeleza kuwa serikali imemtambua Shikuba kama kinara wa usafirishaji wa dawa za kulevya kwa mujibu wa Sheria ya Utambuzi wa Vinara wa Dawa za Kulevya wa Nje (Foreign Narcotics Kingpin Designation Act) ya Marekani. “Hassan (pichani) ni kinara mkubwa wa kimataifa wa dawa za kulevya ambaye anasafirisha mamilioni ya tani za heroine na cocaine kwend...

TRA: Zanzibar kichaka cha kukwepa kodi

Image
Wakati Rais John Magufuli akipambana na wakwepa kodi ili kuhakikisha uchumi wa nchi unakuwa, takwimu za zinaonyesha uwapo wa wafanyabiashara wanaopitisha bidhaa za magendo kwa njia ya panya kati ya mianya 509, Zanzibar inaongoza kwa kuwa na mianya 422,  huku Tanzania Bara ikiwa na mianya 87. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, kuhusu mwenendo wa ukusanyaji wa mapato, matumizi ya mashine za kielektroniki katika ukusanyaji kodi (EFD), kusitishwa kwa bei elekezi na usajili wa vyombo vya moto, Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata, alisema bidhaa hizo hupitishwa Bandari ya Tanga na Mtwara zikitokea Zanzibar. Alisema hali hiyo isipodhibitiwa haraka inaweza kusababisha madhara kwa sababu licha ya Bandari ya Dar es Salaam kuchangia mapato kwa kudhibiti wafanyabaishara wanaokwepa kodi katika kipindi kifupi cha uongozi wa Rais Magufuli, bado kuna haja ya kuandaliwa mazingira rafiki yatakayowabana wakwepa kodi wanaotumia njia hizo ...

9 reasons Buhari’s body language has gone foul

Image
No doubt, there is growing discontent in the country presently, what with the non-availability of fuel, and electricity, plus the economy taking a dive owing to the fall in value of the naira. The optimism that heralded the coming of President Muhammadu Buhari seems to be fast disappearing, giving way to gloom. Immediately after swearing in, Nigerians attributed every little improvement in services in the country to the ‘body language’ of Mr President while every form of dissent or criticism was attributed to the ‘wailing wailers’. What happened to the ‘body language’? As months went by, the miraculous body language of Mr President started losing steam as the situation of Nigeria and Nigerians started taking a turn for the worse. His speeches and actions started to flip flop; denying promises made, trying to explain why it can’t be feasible, or either making a turnaround from statements that had been credited to his administration. Here are nine fl...

Waziri wa Elimu Profesa Ndalichako Aingilia kati Mgogoro wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. Joseph Dar es Salaam

Image
WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako ameingilia kati mgogoro wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. Joseph Dar es Salaam, waliogomea kufanya mitihani na kuwataka warejee madarasani wakati matatizo yao yakishughulikiwa. Wanafunzi hao walikuwa katika siku ya tatu ya mgomo wao jana ambapo pamoja na mambo mengine walikuwa wakilalamikia mapungufu yaliyopo chuoni hapo, ikiwa ni pamoja na maabara za kufanyia mafunzo kwa vitendo, matatizo ya kiutawala, mitaala ya kufundishia pamoja na ada. Profesa Ndalichako aliwasili chuoni hapo jana asubuhi na kukagua mazingira ya kufundishia ya chuo hicho kwa kutembelea maabara zote chuoni hapo na kisha kwenda kuzungumza na utawala, Serikali ya wanafunzi na mwisho alihutubia wanafunzi wote. Ndalichako baada ya kuzungumza na pande zote mbili aliagiza wanafunzi hao warejee madarasani kuendelea na mitihani yao na kuutaka uongozi wa chuo uyafanyie marekebisho mapungufu ya kiutawala yaliyojitoke...

Ndalichako: Vyeti Vya Form Six Vilivyo Katika Mfumo wa GPA Havitabadilishwa Kwenda Division

Image
Serikali imesema haina mpango wa kubadili vyeti vya wanafunzi waliomaliza kidato cha sita mwaka jana kutoka kwenye mfumo wa alama za GPA kwenda Divisheni. Msimamo huo wa serikali, umetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako.   Amesema serikali haina mpango wa kubadili mfumo huo wa vyeti kwani tangu awali wanafunzi walisoma kwa mfumo wa GPA na vyeti vilitoka kwa mfumo huo. “Hatuwezi kubadili vyeti hivyo, isipokuwa vimehitajika kwa ajili ya marekebisho madogo ambayo Katibu Mkuu wa Wizara, aliyasema lakini siyo kubadili kwenda mfumo wa divisheni,” alisema. Februari mwaka huu, Baraza la Taifa la Mitihani (Necta), lilitangaza kusitishwa kwa ugawaji wa vyeti vya kidato cha sita kwa wanafunzi waliohitimu mwaka 2015, huku likiagiza kuwa vile vilivyokwisha gawanywa kwa wahitimu hao vinatakiwa kurejeshwa kwenye chombo hicho. Hata hivyo, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk, Charles Msonde, hakubainisha ...

Baada ya uchaguzi wa Meya Dar kuahirishwa Chadema Watoa Tamko Leo...'Hatutasusia Uchaguzi Mpaka Kieleweke'

Image
Uchaguzi wa Meya Dar es salaam unazidi kuchukua headline kila siku. Ikiwa jana tu Baadhi ya Wabunge na Madiwani wa Ukawa walitinga ofisi ya Halmashauri  ya jiji kutaka kujua tarehe ipi uchaguzi utafanyika lakini hawakupata majibu hayo. Leo March 5 2016Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA‘ Taifa, Freeman Mbowembele ya Waandishi wa habari ameyazungumza haya…. ’Hatutaomba tena kumpata Meya wa jiji la Dar es salaam, tutadai kumpata Meya, Serikali wasifikiri watapanga wao tarehe ya kumchagua Meya, wamekuwa na utaratibu wa kutaka tarehe ya kumchagua Meya kwa kutushtukizia masaa 24 kabla, kanuni inadai siku saba, tutataka tarehe ya kuchagua na siku hiyo atachaguliwa Meya asipochaguliwa Meya siku hiyo tusilaumiane’:-Freeman Mbowe Aidha Mbowe ametoa msimamo wa  chama alipoulizwa kama watasusia uchaguzi, haya ni majibu yake… ’hatuwezi kususia uchaguzi wa Meya kwa sababu ni haki yetu kuongoza jiji kwa sab...

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Nassor Ahmed Mazrui Ahojiwa na Jeshi la Polisi Zanzibar Na Kuachiwa Kwa Dhamana

Image
Wakati polisi visiwani Zanzibar wakimhoji Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui jana, ulinzi uliimarishwa mjini Unguja huku askari wenye silaha na magari ya deraya wakifanya doria mitaani. Mazrui, ambaye alifika makao makuu ya jeshi hilo saa 2:00 asubuhi akiambatana na wakili wake, ndiye aliyekuwa mkuu wa timu ya kampeni ya mgombea urais wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, katika uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2015, ambao chama chake kinaamini kuwa kilishinda. Barabara zinazoelekea makao makuu ya polisi kutokea Jang’ombe, Kilimani na Bomani zilifungwa huku vikosi vya ulinzi na usalama vikiwa vimetapakaa maeneo hayo na mitaa mbalimbali mjini Unguja. Wakazi wa Zanzibar wanaojiandaa kwa uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20, kuanzia Jumatano mchana walishuhudia askari wenye sare wakiwa katika magari maalumu ya kijeshi wakirandaranda kwenye barabara za Unguja, hususan mitaa ya Ng’ambo kupitia Mnazi Mmoja, Darajani, Amani, Chumbuni na Mtoni k...

Choi! Sahara Reporters comes for Dino Melaye...

Image
The senator at plenary today asked Nigerian men to patronize Made-in-Nigeria women...and Sahara Reporters came for him with this...that's Dino's ex-wife!

Kim K steps out in all Yeezy 3 outfit as she meets up with sister Kourtney

Image
Kim Kardashian who seems to be doing well losing her baby weight stepped out in all Yeezy 3 style outfits with her older sister Kourtney Kardashian who wore a dress and a pair of boots. More photos after the cut...