Hatimaye rufaa ya wanamuziki maarufu nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’, imesikilizwa katika Mahakama ya Haki za Binadamu Afrika (AfCPHR) jijini Arusha Machi 11, mwaka huu na sasa zimebaki saa 72 tu kujua hatima yao, yaani Machi 18, 2016, UWAZI linakupa zaidi. Rufaa hiyo ilisikilizwa na mahakama hiyo yenye majaji 11 kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) ambapo rais wao ni Jaji Augustine Ramadhani wa Tanzania ambaye pia aliwahi kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania. MAJAJI WENYE SIRI MOYONI Baadhi ya majaji waliotajwa kusikiliza rufaa hiyo na nchi zao kwenye mabano ni Ben Kioko (Kenya), Solomy Balungi Bassa (Uganda), Duncan Tambala (Malawi), Angelo Vasco Matuse (Msumbiji), Sylvain Ore (Ivory Coast), El Hadji Guisse (Senegal) na Rafaa Ben Achous (Tunisia). KUTOKA MAHAKAMANI Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika kutoka katika mahakama hiyo, rufaa hiyo ilisikilizwa kwa faragha na hakuna mwandishi wa habari yeyote aliyeruhusi...