Posts

Showing posts with the label Siasa

Zitto Kabwe Afunguka Tena Kuhusu Sakata la Rushwa Kamati za Bunge..Awataja Takururu...

Image
Zitto juzi alitangaza kujiuzulu katika Kamati Bunge Huduma za Jamii aliyokuwa akihudumu kwa madai ya baadhi ya wajumbe kupokea rushwa. Kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa 'Facebook' Mbunge Zitto amesema kwamba hatua inayochukuliwa na TAKUKURU ni hatua nzuri itakayopelekea ukweli kujulikana na watakaokutwa na makosa kuchukuliwa hatua stahiki. ''Uchunguzi wa vyombo vya dola ni moja ya njia muafaka ya kuhakikisha kila lisemwalo linakuwa na ukweli na pale ambapo suala limezushwa tu itajulikana na wazushaji hatimaye wataacha''-Amesema Zitto. Aidha ikumbukwe kuwa baada ya tuhuma za rushwa katika kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii Mbunge Zitto Kabwe alimwandikia Spika wa Bunge Job Ndugai barua ya kujiuzulu akifuatiwa na Mbunge wa Nzega Mjini Hussen Bashe (CCM) ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo na ukweli uweze kufahamika.

RC Makonda Aitisha Kikao na Walimu ili Kujadili Matatizo Yanayowakabili

Image
Mkuu  wa Mkoa  wa  Dar  es  Salaam  Paulo  Makonda  amemwagiza Ofisa Elimu,Raymond  Mapunda  kuitisha  mkutano  wa  walimu  March 26 mwaka  huu ili  kujadili matarizo  yanayowakabili likiwemo  la  kutopanda  madaraja  kwa  wakati. Makonda  aliyasema  hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akikabidhi  madawati 500 katika shule  ya  msingi  Kawawa yaliyotolewa  na  kampuni  ya  simu  za  mkononi  ya  Tigo. Mkuu huyo alieleza kuwa yapo matatizo mengi  yanayowakabili walimu yanayotokana  na  watu  wanaojinufaisha matumbo  yao kwa kuwalipa walimu hewa Katika hatua nyingine,Makonda aliwataka walimu kutovunjwa moyo kutokana na matatizo yaliyopo katika sekta  ya  Elimu. Naye mkurugenzi wa kampuni ya Tigo,Diego Gutierrez alisema kuwa mchango huo ni...

CCM na CUF Watwangana Ngumi Pemba Wakati Wakisherehekea Ushindi wa Dr. Shein

Image
Jeshi la Polisi jana walitumia mabomu ya machozi kurejesha hali ya amani baada ya wananchi kuanza kupigana kwa sababu za kisiasa wakati wakisherehekea ushindi wa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, katika kijiji cha Mjini Wingwi Wilaya ya Micheweni, Pemba. Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Micheweni, Rashid Khalid Salim, alidai vurugu hizo zimesababishwa na wanachama wa CCM kutoka katika kijiji cha Kwale wilayani humo. Alisema baada ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec) kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa marudio, wanachama wa CCM katika kijiji cha Kwale, walianza kukusanyika na ngoma zao na kuanza safari ya kuingia katika kijiji cha Mjini Wingi, sehemu ambayo ni ngome ya wanachama wa CUF, huku wakisherehekea kwa kurusha 'vijembe' (maneno ya kejeli) na matusi. “Pamoja na kutakiwa kuacha matusi wakati wakisherehekea ushindi wa Dk. Shein, waliendelea na kusababisha wenzao kupandwa na ghadhabu kuwachemka na kuanza kupigana,” alisema Mwenyeki...

Chadema Yawafuata CCM Mahakamani....Yapinga Agizo la Jiji La Dar Kuwazuia Wananchi Kuingia Kwenye Ukumbi wa Uchaguzi wa Meya

Image
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema hakikubaliani na agizo la serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Jiji la kuwataka wanaotakiwa kuhudhuria kwenye kikao cha uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es salaam wawe ni wajumbe pekee watakaopiga kura. Chama hicho kimekataa agizo hilo na badala yake kinataka wananchi wote wa jiji la Dar es salaam wahudhurie katika kikao hicho. Msimamo huo wa Chadema unapingana na barua ya wito wa mkutano wa uchaguzi huo iliyoandikwa Machi 15, 2016 na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sarah Yohana, iliyosema kuwa watakaoruhusiwa kuingia katika viwanja hivyo ni wajumbe pekee ambao ni wapigakura.  Akizungumza na wanahabari jana jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Mwita Waitara alisema sheria na kanuni zinaruhusu wananchi kushiriki kikao hicho cha wazi, hivyo Yohana hana mamlaka ya kuwazuia. “Sisi tunafuata sheria na kanuni, barua ya mkurugenzi inaeleza kinyume cha utaratibu,” alise...

Maandalizi ya Uchaguzi Visiwani Pemba Yakamilika....Wananchi Watakiwa Kujitokeza Kwa Wingi Kesho Kupiga Kura

Image
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), imesema maandalizi ya uchaguzi visiwani Pemba yamekamilika na kuwataka wananchi kujitokeza kesho kupiga kura na kuachana na dhana kuwa kutakuwa na vurugu. Mwandishi wetu alishuhudia malori saba ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) yakipakia vifaa vya uchaguzi katika ofisi ya ZEC Pemba katika tukio lililowafanya baadhi ya wananchi kuacha shughuli zao wakishangaa na wengine wakisema; “sasa shughuli imeanza”. Ofisa Mdhamini wa ZEC Pemba, Ali Mohammed Dadi alisema wameshapokea karatasi na masanduku ya kupigia kura na fomu mbalimbali. Alisema karatasi za uchaguzi wa wawakilishi na madiwani zilianza kusambazwa jana na walitarajia kupokea za urais jana jioni na kuzisambaza leo. Jana, magari 15 ya polisi aina ya Land Rover yakiwa na askari 10 wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kila moja, zilionekana zikirandaranda katika mitaa ya Pemba. “Sisi tunachotaka ni amani tu hao askari waje tu watulinde hakuna mfanya vurugu hapa. Hata...

Maalim Seif Aiondoa Familia yake Zanzibar na Kuipeleka Muscat Oman

Image
Pichani ni mkewe Seif Shariff Hamad, Bi Awena Sinani Masoud akiwa chumba cha VIP uwanja wa ndege na tiketi yake ya Oman Air, muda mfupi kabla ya kuondoka. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Seif Shariff Hamad ameondosha familia yake katika Kisiwa cha Unguja na kuipeleka Muscat-Oman. Familia hiyo ya Maalim Seif Shariff Hamad wameondoka jioni hii kwa kutumia ndege ya Shirika la ndege la Oman (Omar Air). Familia hiyo ya Maalim Seif wameondoka katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Airport saa 5:50 jioni hii. Haikuweza kufahamika mara moja sababu hasa za Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Seif Shariff Hamad kuiondoa familia yake Zanzibar. Kwa sasa Makamu huyo wa Kwanza wa Rais yupo katika mapumziko katika Hoteli ya Kitalii ya Dar es Salaam Serena. Chanzo: ZanzibarNews.net

Ripoti: Kama Donald Trump Atashinda Urais Marekani ni Hatari Kwa Dunia...Soma Hapa Kwanini..

Image
Shirika moja la kimataifa limesema ushindi wa Donald Trump unachukuliwa kuwa miongoni mwa hatari 10 kuu zaidi zinazokabili dunia. Shirika hilo la Economist Intelligence Unit linaonya kuwa iwapo Bw Trump atashinda urais Marekani, hilo huenda likavuruga uchumi wa dunia na kuongeza hatari za kisiasa na kiusalama dhidi ya Marekani. Hata hivyo, shirika hilo halimtarajii Bw Trump, anayeongoza kwenye kinyang’anyiro cha kumchagua atakayepeperusha bendera ya chama cha Republican, kumshinda Bi Hillary Clinton ambaye shirika hilo linasema "ana uwezekano mkubwa sana kuwa mgombea wa chama cha Democratic". Ushindi wa Trump unaorodheshwa kuwa hatari zaidi kwa dunia kushinda hata Uingereza kuondoka kutoka kwa Umoja wa Ulaya au hata makabiliano ya kivita katika bahari ya South China Sea. Kuyumba kwa uchumi wa Uchina au Urusi kuingilia kivita Ukraine na Syria na kusababisha “vita baridi” vipya ni miongoni mwa mambo ambayo yanachukuliwa kuwa hatari zaidi ya ...

Rais Magufuli Akerwa Na Mikataba Mibovu Ya Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL....Aeleza Kilichomfanya Amrudishe Profesa Muhongo Wizara ya Nishati

Image
Rais John Magufuli jana aliitaja kampuni ya kuzalisha umeme ya IPTL wakati akizungumzia matatizo yanayosababishwa na kununua umeme unaozalishwa na mitambo ya kukodi na kupiga marufuku mikataba hiyo. Rais pia alipuuzia shutuma zinazorushwa dhidi ya Profesa Sospeter Muhongo, ambaye alijiuzulu wadhifa wa Waziri wa Nishati na Madini kutokana na sakata la IPTL, akisema “wakati mwingine vitu vizuri hupigwa vita” na hivyo amemrejesha mbunge huyo wa Musoma Vijijini kwenye wizara hiyo kwa sababu ya uchapakazi na si siasa.  Tangu aingie madarakani, Rais Magufuli amekuwa akifichua kashfa za ufisadi ambazo hazikuwahi kujadiliwa vikali katika utawala uliopita, lakini jana alitoa mfano wa IPTL kama moja ya mikataba iliyoisababishia Serikali matatizo. Kashfa zilizoikumba sekta hiyo ni pamoja na mkataba wa uzalishaji umeme na kampuni ya Richmond Development iliyodhihirika baadaye kuwa haikuwa na uwezo, uchotwaji wa zaidi ya Sh300 bilioni kutoka kwenye Akaunti ya...

Tazama Video: Rais Magufuli awapa Siku 15 Wakuuu Wa Mikoa Kuondoa Majina ya Wafanyakazi Hewa Wanaolipwa Mishahara

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amesema jumla ya wafanyakazi 202 katika halmashauri 14 katika mikoa ya Singida na Dodoma waligundulika kuwa hewa na kulipwa mishahara kila mwezi. Rais ameyasema hayo alipokuwa akiwakumbusha wakuu wa kikoa wapya ambao amewaapisha leo Ikulu jijini Dar es salaam. ''Kwa mikoa miwili tuu wafanyakazi hao 202 wanalipwa mishahara hewa na kwenye data ilionyesha wengine wamefariki, wamestaafu, wamefukuzwa , wengine likizo bila malipo wote hao kumbe wanalipwa malipo ya serikali fedha ambazo zingetumika kutatua matatizo ya wananchi''. Amesema Rais Magufuli Kwa msingi huo kwa halmashauri 180 nchini ina maana kwa mahesabu ya haraka haraka kuna wafanyakazi 2000 na zaidi wanalipwa mishahara hewa. Hivyo Rais Dkt Magufuli ametoa agizo kwa wakurugenzi wa taasisi za serikali kuanzia leo ndani ya siku 15 kuhakikisha wanapitia majina ya waajiriwa wote wa serikali na kuondoa majina ya ambao wana...

Picha : Rais Magufuli Awaapisha Wakuu Wapya Wa Mikoa Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Jeshi la Polisi,Zelote Steven Zelote kuwa mkuu wa mkoa wa Rukwa,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu kuwa mkuu wa mkoa wa Kagera,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga  kuwa mkuu wa mkoa wa Katavi,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali M...

Rais Magufuli Ataka Vijana Waache Kucheza Pool table na Badala Yake Wafanye Kazi.....Asiyetaka ALAZIMISHWE na Ikibidi Apelekwe Kambini Akafanye Kazi

Image
Rais John Magufuli leo amewaapisha wakuu wa mikoa wapya aliowateua hivi karibuni na katika hotuba yake amewataka wakuu wa mikoa hao wapya kuhakikisha vijana wanafanya kazi na kuacha uzembe.   Rais Magufuli amewataka wakuu wa mikoa hao kuhakikisha hakuna vijana ambao watakuwa wanakwenda kucheza pool table asubuhi na badala yake vijana hao wanatakiwa kufanya kazi kweli kweli hata kwa kulazimishwa. "Nimeamua kuwateua wakuu wa mikoa nikiamini kwamba mtaniwakilisha vizuri katika mikoa yenu . " Napenda niwape pole kwa sababu mtakwenda kufanya kazi kweli kweli kutatua kero za wananchi wetu. " Lakini pia niwaombe wakuu wa mikoa mkasimamie watu wafanye kazi hasa vijana . "H aiwezekani vijana leo hii una wa kuta saa mbili asubuhi wanacheza Pool table wakati wakina mama wanalima shambani, kama hawataki kufanya kazi kwa kupenda walazimishwe kufanya kazi. Atakayekataa mpelekeni  kambini akafanye kazi" amesema Rais Magufuli Rais Magufuli...

Msomi Prof Baregu Aibuka na Kudai Utawala wa RAIS Magufuli ni wa Kejeshi...Kuwapo Kwa Wanajeshi Wengi Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa Wamtisha

Image
SIKU moja baada ya Rais Dk. John Magufuli kuteua wakuu wa mikoa wapya, mtaalamu wa sayansi ya siasa, Profesa Mwesiga Baregu, ameibuka na kusema kuwa kuwapo kwa wanajeshi wengi wastaafu katika uteuzi huo inadhihirisha wazi kuna dalili za utawala wa kijeshi nchini. Profesa Baregu amesema kuwa  wanajeshi huwa hawana hulka ya kidemokrasia. “Kitu kimoja kinachojitokeza kwenye uteuzi huu ni kuwepo kwa wanajeshi wastaafu, na mimi ninavyoelewa wanajeshi huwa hawana hulka za kidemokrasia. Hii inaonyesha wazi kwamba utawala huu ni wa kijeshi,” alisema. Profesa Baregu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alisema haileti picha nzuri kuwapo kwa wanajeshi wengi katika utawala kwa sababu tawala za mikoa na wilaya ni saula la kiraia na demokrasia zaidi. Alisema rasimu ya katiba ambayo yeye alikuwa mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ilipendekeza kupitia upya tawala za mikoa na kupunguza idad...

Ester Bulaya Apeta Tena Mahakamani....Pingamizi La Stephen Wassira Latupiliwa Mbali

Image
Mahakamaa Kuu Kanda ya Mwanza, imetupilia mbali maombi ya baadhi ya wapigakura wa Jimbo la Bunda Mjini ya kuruhusiwa kukata rufaa kupinga uamuzi wa Makahama Kuu wa kufuta shauri lao la kupinga matokeo ya uchaguzi. Maombi hayo yaliwasilishwa na Magambo Masato na wenzake wanne wanaompigania Stephen Wassira, wakiiomba mahakama hiyo kuwaruhusu kukata rufaa Mahakama ya Rufani baada ya kutoridhiswa na uamuzi ya kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana yaliyompa ushindi Ester Bulaya (Chadema), dhidi ya Stephen Wasira (CCM). Jaji anayesikiliza shauri hilo namba 25 la mwaka 2016, Rose Ebrahim alisema jana kuwa anakubaliana na pingamizi lililowekwa na wajibu maombi kuwa hayana mashiko kisheria. Pingamizi hilo lilowasilishwa na Wakili Mfawidhi wa Serikali, Paschael Marungu alidai aliyesaini hati ya maombi siyo aliyethibitisha kwani hilo ni kosa la kisheria. Wakili Marungu alidai hati hiyo ilisaniwa na Wakili Denis Kahangwa na kuthibitishwa ...

Siri Imefichuka...CUF Watoa Sababu za Maalim Seif Sharif Hamad Kuishi Serena Hoteli Pamoja na Gharama Iliyotumika Hadi sasa

Image
SIRI imefichuka kuhusu hatua ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar (SUK), Maalim Seif Sharif Hamad, kuishi hotelini jijini Dar es Salaam. Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), amekuwa akiishi katika Hoteli ya Serena jijini Dar tangu aliporuhusiwa kutoka Hospitali ya Hindu Mandal Machi 8, mwaka huu alipokuwa amelazwa kwa matibabu. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mmoja wa ofisa wa ngazi za juu wa CUF, alishangazwa na hatua ya baadhi ya watu kuhoji kiongozi huyo kuendelea kuishi hotelini hapo. Alisema hatua ya kiongozi huyo kuishi hotelini ni matokeo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), kushindwa kutekeleza ahadi ya kumpa nyumba pindi anapokuwa Dar es Salaam katika shughuli zake. Alisema kutokana na hali hiyo imekuwa ni utaratibu kwa kiongozi huyo kufikia katika hoteli hiyo na gharama za kuishi hotelini hapo hulipwa na SMZ kwa mujibu wa sheria. “Tangu mwaka 2010 M...

Picha 12 za Mkutano wa Hadhara wa Kumtambulisha Katibu mkuu CHADEMA Dr Vicent Mashinji -Furahisha Mwanza

Image
Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Vicent Mashinji, jana alitambulishwa rrasmi kwa wakazi wa Mwanza kwenye uwanja wa furahisha. Viongozi mbalimbali wa kitaifa wa Chadema pamoja na baadhi ya Wabunge kutoka Chadema walikuwepo kuushuhudia utambulisho huo wa Katibu Mkuu wao kwa wananchi.

Breaking News: Rais Magufuli Afanya Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa 26....Kati Yao 13 ni Wapya, 7 Wamebakizwa na 5 Wamehamishwa

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa wakuu wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara, ambapo kati yao 13 ni wapya, 7 wamebakizwa katika vituo vyao vya kazi, 5 wamehamishwa vituo vya kazi na 1 amepangiwa Mkoa Mpya wa Songwe. Uteuzi huo umetangazwa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe leo tarehe 13 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.   Wakuu wa Mikoa walioteuliwa ni kama ifuatavyo; Mh. Paul Makonda -  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam. Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga  - Mkuu wa Mkoa wa Geita. Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu  - Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga  - Mkuu wa Mkoa wa Katavi. Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga  - Mkuu wa Mkoa wa Kigoma. Mh. Godfrey Zambi  - Mkuu wa Mkoa wa Lindi. Dkt. Steven Kebwe  - Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Kamishna Mstaafu wa Polisi Zerote Steven  - Mkuu wa Mkoa w...

Mbunge wa CCM Faustine Ndugalile Awakosoa Mawaziri wa Rais Magufuli

Image
Mbunge  wa Kigamboni, Dar es Salaam ,Faustine Ndugalile (CCM) amekosoa utendaji wa mawaziri wa serikali ya Rais Magufuli  akisema wanatishia wafanyakazi badala ya kuwaelekeza katika utendaji wao. Katika ujumbe aliouweka kwenye mtandao wa twitter kwa lugha ya kiingereza, Ndugalile ameandika: "Ministers should encourage or provide practical solutions to problems instead of barking orders and terrorizing civil servants."  Kwa lugha ya kiswahili, mbunge huyo alimaanisha: " Mawaziri wanatakiwa kuwatia moyo au kutoa suluhisho kwa matatizo badala ya kufoka na kuwatisha watumishi wa umma." Alipoulizwa kuhusu ujumbe huo,Ndugalile alikiri kuwa ni wake na kusisitiza kuwa ni wajibu wake kama mbunge kuisimamia serikali. "Mimi ni mbunge, kazi  ya  mbunge ni kuisimamia serikali.Ikifanya vizuri tutaisifia, ikikosea tutaikosoa. "Nimesema baadhi  ya  mawaziri- sio wote wanawatisha wafanyakazi. Kazi ya kiongozi ni kuonyesha uongoz...