BASI LA NEW FORCE LAPATA AJALI NA KUUA WATU 12 KITONGA IRINGA
Watu
12 wamefariki dunia papo hapo baada ya lori la mbao lililokuwa
likitokea njombe kwenda jijini Dar es Salaam kupasuka tairi na kugongana
na basi la abiria la new force lililokuwa linatokea jijini Dar es
Salaam kuelekea tunduma hii leo katika eneo la kitonga wilaya ya kilolo
mkoani iringa.
Kwa
mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa iringa, kamishina msaidizi wa
polisi Ramadhani Mungi amesema kuwa waliokufa ni wanaume nane na
wanawake wanne majeruhi ni 28 ambao wengine wamepelekwa iringa mjini na
wengine wako katika hospitali ya wilaya kilolo-iringa.
Aidha
Kamanda Mungi amewataka madereva kuwa makini hasa katika kipindi hiki
cha sikukuu na kuepuka mwendo kasi pamoja na kutoa taarifa pale vitendo
kama hivyo vinapotokea



Comments
Post a Comment