BAADA YA KUTOA MAREKANI MTOTO GETRUDA CLEMENT AKARIBISHWA BUNGENI LEO.
Getrude
Clement mwenye umri wa miaka 16 ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu
anayesoma shule ya Sekondari Mnarani iliyopo jijini Mwanza, leo amepata nafasi
ya kufika bungeni Dodoma baada ya kupewa mwaliko wa Serikali
Hivi karibuni Getrude alihutubia viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika New York Marekani ambapo leo Bungeni amewahimiza Watanzania kutunza mazingira na kufuata maelekezo yanayotolewa na Serikali na wataalamu wa mazingira ili kuyatunza mazingira wanamoishi.

amesema kuwa amefarijika kwa kuwawakilisha vijana wa Tanzania na dunia kwenye
mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi ambapo mataifa 175 yalikutana kusaini
makubaliano ya Paris.
Katika
kuwahimiza vijana kujenga tabia ya kutunza mazingira, Getrude amewaasa vijana
hasa wanafunzi kusimamia suala la utunzaji wa mazingira wakiwa shuleni kwa kwa
kujiunga na klabu mbalimbali ambapo yeye amejiunga na klabu ya “Mali Hai”
iliyopo shuleni anaposoma.
Kwa upande
wa Watanzania kwa ujumla kwenye utunzaji wa mazingira, Getrude amesema kuwa ni
vema wajifunze kutoka mataifa mengine yanavyosimamia utunzaji wa mazingira hasa
matumizi ya mifuko ya plastiki.
Mwanafunzi
huyo amekaribishwa na kutambulishwa kwa wabunge leo mjini Dodoma kwa heshima ya
kuliwakilisha vema taifa wakati wa utiaji saini makubaliano ya namna ya
kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa
Ban Ki moon alimkaribisha Getrude kwa viongozi hao na kusema “Ni furaha
yangu kumualika Getrude Clement ambaye pia ni mwakilishi wa vijana anayeishi
Tanzania na anaziwakilisha sauti za vijana”.
Comments
Post a Comment