Watu Wanne Watiwa Mbaroni Kwa Tuhuma za Kutumia Jina la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kutapeli
Watu wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
wakikabiliwa na tuhuma za kujipatia fedha kwa kutumia jina la Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa.
Washtakiwa hao walifikishwa katika
mahakama hiyo jana kujibu mashtaka 12 yanayowakabili, likiwamo la
kughushi barua na kuziwasilisha katika vituo vya mafuta wakirubuni
watumiwe kiasi cha fedha ili waweze kupata punguzo la kodi.
Washtakiwa hao ni mwanafunzi, Issa Mohamed Awadhi (27)
maarufu
kama Charles Robert au Mwamunyange, mkazi wa Ilala, ambaye hakuwapo
mahakamani hapo kutokana na kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
(MNH) baada ya kuugua.
Wengine ni Hamisi Tembo(37) mkazi
wa Ilala, mtengeneza mihuri, Nicolaus Obado(32), mkazi wa Mbagala Kuu
na Wakati Mungi (51) mfanyabiashara na mkazi wa Yombo Makangarawe.
Washtakiwa walikana mashtaka na upande wa mashtaka ulidai upelelezi haujakamilika na kukosa dhamana. Kesi itaendelea Aprili 11.
Comments
Post a Comment