Posts
Showing posts from March, 2016
Mkoa wa Mwanza Waongoza Kuwa na Watumishi Hewa Wengi Serekalini Ukifuatiwa na Mkoa wa Arusha...Habari Nzima Ipo Hapa
- Get link
- X
- Other Apps
Mkoa wa Mwanza waongoza kuwa na watumishi hewa 334 ukifuatiwa na Mkoa wa Arusha kwa kuwa na watumishi hewa 270 ikiwa nchi nzima na watumishi hewa 2,702. Hata hivyo Shinyanga na Songwe ni mikoa isiyo kuwa na watumishi hewa. Sababu kubwa iliyoiwezesha smShinyanga kutokua na watumishi ni matokei ya mikakati ya mkoa hu kupeleka majina ya watu wanaostahili kulipwa mishahara kila mwezi. Akizungumza na Wakuu wa Mikoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene aliwataka wakuu wa mikoa wafanye kazi ikiwemo ubunifu wa miradi ya kuongeza mapato.
Binti Mrembo Ajinyonga Kwa Kamba Hadi Kufa..Aacha Ujumbe Mzito..Usome Hapa
- Get link
- X
- Other Apps
Binti mmoja anayejulikana kwa jina la Jesca ambaye ni mfanyakazi wa Longido Mountain Lodge amekutwa amejinyonga katika hotel ya Longido Mountain Lodge akiacha ujumbe kuwa kifo chake kisihusishwe na mtu yeyote amejinyonga kwa ridhaa yake mwenyew akiacha ujumbe wa majina ya watu anao wadai walipe madeni yake kabla ya kusafirishwa kwao pamoja na namba za Mama yake mzazi.
Diamond: Sina Tatizo na Msanii yoyote Hata Ukija Ofisini Kwangu Utakuta Nimebandika Picha ya Alikiba na Mr.blue
- Get link
- X
- Other Apps
Diamond amesema hataki kuulizwa tena kama ana bifu na msanii mwingine, amedai hana tatizo na msanii yoyote na ndio maana hata ukienda ofisini kwake utakuta ameweka picha za wasanii wote hata ambao amekuwa akihusishwa kuwa na bifu nao. “Ukija ofisini kwangu me nna kuna picha ya blue nimembandika, kuna picha ya Juma Nature, kuna picha ya Ali , kuna picha ya Prof, Jay, kuna picha ya Ray C, kuna picha ya Q chief, TID, AY, wasanii wote wakubwa ambao anajua walianza katika huu muziki, wana mchango katika huu muziki wote me nimewaweka” Diamond Alisema “Ofisini kwangu tu ukiingia tu reception, ukiingia tu kunasehemu nimeweka picha za wasanii wote , siwezi kuweka wote kwasababu zisingetosha lakini kuna baadhi ya wasanii nimeweka kwasababu najua wanamchango kwenye soko la muziki wa Tanzania.” Diamond alielezea Diamond pia amesema kuwa yeye ndio huwa anahushishwa na bifu na wasanii wengine lakini yeye hana tatizo na mtu
Mwimbaji Vanessa Mdee Amfungukia Laivu Jack Patrick Aliyoko Jela....
- Get link
- X
- Other Apps
Baada ya kumkwapua Juma Mussa Mpolopoto ‘Jux’ aliyekuwa mpenzi wa modo Jacqueline Fitzpatrick ‘Jack Cliff’ kisha modo huyo kufungwa kwa msala wa madawa ya kulevya nchini China, mtoto mzuri wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘V-Money’ ameibuka na kumzungumzia ‘mtalaka’ huyo wa Jux. V-Money alimfungukia modo huyo mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa akifanya mahojiano maalum (exclusive) na Global TV Online ambapo pamoja na mambo mengine ya kimuziki, staa huyo anayetamba na Wimbo wa Niroge, alitumia dakika kadhaa kufafanua tuhuma zinazoelekezwa kwake kuhusiana na Jack. Awali, wanahabari wa Global TV walianza kumuuliza kama alikuwa akimfahamu Jack tangu alipokuwa ana uhusiano wa kimapenzi na Jux ambapo Vanessa alijibu kuwa alikuwa hamfahamu. “Jack nilikuwa sifahamiani naye. Nilikua namjua tu ni msichana anayefanya music video na nilikuwa naona kazi zake za umodo,” alisema Vanessa kwa kujiamini. Alipoulizwa anazungumziaje kama endapo Jack atakuwa anaumia kule
Mbunge Sugu Awachana Wasanii Kufanya Show Ulaya....Adai Sio Kigezo Kwa Music Wetu Kukua
- Get link
- X
- Other Apps
Kwenye stori tatu ya Planet Bongo ya East Africa Radio, Sugu amesema huwezi kutumia kigezo cha wasanii kufanya show nje ya Afrika yaani Ulaya, America na kwengineko kama kigezo kuwa game imekua, kwa sababu show kama hizo walishazifanya miaka zaidi ya 20 iliopita. “Huwezi kutoa credit kwa kusema wasanii wanaenda kupiga show Ulaya, Sugu, X-plastars, tumekwenda tour Europe miaka 20 iliyopita 18 au 17, kwa hiyo mimi sichukulii hiyo kama credit kama tour tulizokuwa tunapiga sisi, I apriciate hustle za kila mtu lakini sisi tulikuwa tunaenda kwenye mafestival ya dunia unapiga mbele ya mtu laki moja, ukirudi nyumbani hakuna suport kwa hiyo ili watu laki moja waliokuona kule wakupe thamani wanakuja kuangalia huko kwenu huko vipi unakuta watu wanakuzingua tu”, alisema Sugu. Sugu kwa sasa ameachia wimbo wake unaoitwa freedom, baada ya kimya kirefu kilichosababishwa na yeye kuingia kwenye siasa, mpaka kufanikiwa kutwaa jimbo la Mbeya mjini.
Waziri wa Mambo ya nje, Balozi Mahiga Asema Serikali imesikitishwa na Kusitishwa kwa Msaada wa Mabilioni ya Marekani
- Get link
- X
- Other Apps
Serikali imeeleza kusikitishwa na uamuzi wa Marekani kusitisha uhusiano katika Shirika la Changamoto za Milenia (MCC), bila kuishirikisha wala kuisikiliza. Kadhalika, imesema hakuna umuhimu wa misaada ya afya na elimu inayofadhiliwa na Marekani kwa dola za Marekani milioni 700 (Sh. trilioni 1.5), kama imejitoa katika kusaidia miradi ya umeme ambayo ni muhimu katika utekelezaji wa miradi inayofadhili, kwa kuwa ni sawa na kutoa kwa mkono wa kulia na kupora kwa mkono wa kushoto. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, baada ya kupokea taarifa ya uamuzi wa MCC, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga, alisema uhusiano na Marekani utaendelea katika maeneo mengine, lakini kwa fedha hizo hakuna la kufanya ingawa milango iko wazi iwapo watafikiria upya. “Fedha ni zao, uamuzi ni wao wameutoa Washington. Hatuwezi kulia kwa ajili ya hili, tutaendeleza ushirikiano katika maeneo
Zitto Kabwe: Tanzania Kunyimwa Fedha ni Matokeo ya Ubabe wa CCM
- Get link
- X
- Other Apps
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, amesema MCC kuinyima fedha Tanzania ni kwa sababu ya ubabe wa CCM na kwamba, sasa watu wasivikwe koti la uzalendo kwa jambo hilo. Kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook, Zitto aliandika kuwa: “Uzalendo ni kutaka haki ya kidemokrasia Zanzibar. Haki ya Wananchi waliochagua viongozi wao Oktoba 25, 2015. “Sitakubali kuvishwa koti la uzalendo kwenye suala la MCC. Hilo ni suala la CCM, kukosa misaada ya Marekani ni matokeo ya ubabe wa CCM kuhusu Zanzibar. “Haina mahusiano yeyote na uhuru wa nchi yangu. Nawasihi Wazanzibari wawe na subra Mola kamwe hatawatupa. Haki itapatikana tu. Nawasihi Watanzania kuelewa kwamba CCM ndio imetufikisha hapa na iubebe mzigo huu bila kuufanya ni mzigo wa nchi.” Aliandika pia kwamba: “Zanzibar inatazamwa kama Zanzibar, kwa wenye maono mafupi. Nilipata kuwaambia viongozi wenzangu kwamba tishio kubwa zaidi la kutoshughulikia mtanziko wa Zanzibar ni upotosh
Watu Wanne Watiwa Mbaroni Kwa Tuhuma za Kutumia Jina la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kutapeli
- Get link
- X
- Other Apps
Watu wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na tuhuma za kujipatia fedha kwa kutumia jina la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Washtakiwa hao walifikishwa katika mahakama hiyo jana kujibu mashtaka 12 yanayowakabili, likiwamo la kughushi barua na kuziwasilisha katika vituo vya mafuta wakirubuni watumiwe kiasi cha fedha ili waweze kupata punguzo la kodi. Washtakiwa hao ni mwanafunzi, Issa Mohamed Awadhi (27) maarufu kama Charles Robert au Mwamunyange, mkazi wa Ilala, ambaye hakuwapo mahakamani hapo kutokana na kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) baada ya kuugua. Wengine ni Hamisi Tembo(37) mkazi wa Ilala, mtengeneza mihuri, Nicolaus Obado(32), mkazi wa Mbagala Kuu na Wakati Mungi (51) mfanyabiashara na mkazi wa Yombo Makangarawe. Washtakiwa walikana mashtaka na upande wa mashtaka ulidai upelelezi haujakamilika na kukosa dhamana. Kesi itaendelea Aprili 11.
Wafanyakazi watatu TANESCO Watiwa Mbaroni Kufuatia Kifo cha Mfanyakazi Mwenzao Aliyenaswa na Umeme Juu ya Nguzo
- Get link
- X
- Other Apps
Wafanyakazi watatu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) mkoani Morogoro, wanashikiliwa na Polisi wakihojiwa kutokana na kifo cha mfanyakazi mwenzao, Deo Elias (30), mkazi wa Mazimbu, Manispaa ya Morogoro kwa kunaswa na umeme juu ya nguzo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 5.30 asubuhi maeneo ya Mafiga, wakati Elias akiwa na wafanyakazi wenzake katika eneo la kazi. Kamanda Matei alisema Elias alipokuwa na wenzake katika eneo hilo wakirekebisha umeme, alinaswa na kufa papo hapo. Meneja wa Tanesco Mkoa wa Morogoro, Mhandisi John Bandiye akizungumzia tukio hilo ofisini kwake jana, alisema Elias alikuwa katika kazi za kawaida kama fundi na tukio hilo limetokea kwa bahati mbaya. Mhandisi Bandiye alisema mfanyakazi huyo alikuwa akirekebisha njia ya umeme ya Ngazengwa iliyopo eneo la Mafiga na ilikuwa imezimwa, lakini cha kushangazwa ilikuwa na ume
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya March 30
- Get link
- X
- Other Apps