NEWWWWWS: 71 WATIWA MBARONI NA JESHI LA POLISI !! WAMEAFANYA NINI INGIA HAPAAAA KUJUA ZAIDI.
JESHI
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limesema limewakamata watu
71, silaha nne na dawa za kulevya katika oparesheni ya mwishoni mwa
mwaka.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kamishna wa Polisi Kanda
hiyo, Suleiman Kova alisema Desemba 24 mwaka huu, maeneo ya Ubungo Kibo,
Kinondoni, Polisi walipata taarifa kutoka kwa mwananchi ambapo
walifanikiwa kumkamata mfanyabiashara, Peter Massawe (25).
Kova
alisema Massawe ni mfanyabiashara wa duka la nguo na mkazi wa Ubungo
Rombo alikutwa na bastola aina ya Taurus, yenye namba 801340
iliyotengenezwa nchini Brazil ikiwa na risasi mbili na maganda ya risasi
matatu.
Kwa
mujibu wa Kova, mtuhumiwa alipohojiwa alidai kuwa silaha hiyo ililetwa
na Ismail Mcharo (29), dereva wa bodaboda, mkazi wa Kimara Kilungule kwa
ajili ya hifadhi baada ya kuitumia katika tukio la uporaji lililotokea
maeneo ya Selander Bridge.
Pia
alisema watuhumiwa wengine waliokamatwa ni Matola Rashid (30) muuza
mkaa na mkazi wa Kimara Baruti na Fitina Ramadhan (43) mkazi wa
Magomeni.
‘’Mahojiano
hayo pia yalisaidia kupatikana kwa silaha nyingine ambazo ni shotgun
mbili, bastola moja, pikipiki tatu na simu mbili za mkononi,’’ alisema Kova.
Alisema
watuhumiwa wanahojiwa na kwamba upelelezi wa shauri hilo
utakapokamilika jalada la kesi litapelekwa kwa mwanasheria wa serikali
ili sheria ichukue mkondo wake.
Alifafanua
kuwa jeshi hilo linaendelea kukabiliana na athari za dawa za kulevya
ambapo jumla ya watuhumiwa 68 ambao ni wasambazaji wa dawa hizo,
walikamatwa.
Aidha,
wamekamata magunia manne ya bangi, kete 236 na misokoto 174, mtambo wa
kutengenezea gongo pamoja na lita 50 za pombe haramu ya gongo.
Comments
Post a Comment