TIMU YA TAIFA YA VIJANA WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 15 U15 YAINGIA KAMBINI
Timu
ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15) imeingia kambini
jana jioni katika hosteli za TFF zilizopo Karume jijini Dar es salaam,
kujiandaa na ziara ya mafunzo katika ukanda wa Afrika Mashariki
itakayoanza Disemba Mosi mwaka huu.
Kocha wa timu hiyo Sebastian
Mkomwa amesema vijana wote wameshawasili jijini Dar es salaam na leo
wameanza mazoezi asubuhi katika uwanja wa Karume watakapokua wanajifua
kila asubuhi na jioni mpaka siku ya safari.
Kikosi cha wachezaji 24 kimeingia
kambini kujifua na ziara ya Afrika Mashariki, ambapo timu hiyo
inaandaliwa kwa ajili ya kushiriki kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa
Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17, zitakazofanyika mwaka
2017 nchini Madagascar.
Timu ya Taifa ya vijana imeakua na
program ya kukutana kila mwisho wa mwezi kwa ajili ya kufanya mazoezi
na kucheza michezo ya kirafiki na timu za kombani za U15 katika mikoa
mbalimbali nchini, ambapo kwe mwezi Disemba itakua pamoja kwa wiki tatu
katika nchi za Afrika Mashariki ikicheza michezo ya kirafiki.
Disemba Mosi, U-15 itasasiri
kuelekea jijini Mwanza ambapo itacheza mchezo mmoja wa kirafiki na
kombani ya jijini Mwanza (U17), kasha kusafiri kueleka mkoani Kigoma
itakapocheza michezo miwili dhidi ya kombaini ya mkoa wa Kigoma (U17) na
timu ya Taifa ya Burundi (U17).
Ziara hiyo itaendelea katika jiji
la Kigali kwa kucheza michezo miwili dhidi ya timu ya Taifa ya Rwanda
(U17), Jinja dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda (U17), Nairobi dhidi ya
timu ya Taifa ya Kenya (U17) na kumalizia kwa mchezo dhidi ya kombaini
ya mkoa wa Arusha (U17) na kurudi jijini Dar es salaam.
Comments
Post a Comment