Muhimbili yapatiwa msaada wa vifaa vya kuokoa maisha ya watoto
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) Tanzania, Dk Juma Gulaid akisoma
taarifa kabla ya kukabidhi vifaa vya kuhudumia watoto katika hafla fupi
iliyofanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). Kushoto ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando.Picha
zote kwa hisani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Baadhi ya wauguzi wakisimsikiliza
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF)
Tanzania, Dk Juma Gulaid katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando akizungumza katika hafla ya kupokea
vifaa vya kisasa vya kuhudumia watoto katika hospitali hiyo. Vifaa
hivyo vimekabidhiwa na Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Dk Juma Gulaid.
Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Dk
Juma Gulaid akimkabidhi hati ya vifaa vya kuwahudumia watoto kwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru akipokea
hati ya vifaa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii, Dk Donan Mmbando. Vifaa hivyo vimetolewa na UNICEF.
Baadhi ya wauguzi wakisimsikiliza
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF)
Tanzania, Dk Juma Gulaid katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa
………………………………………………………………………………….
Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH) imepatiwa msaada wa vifaa kumi vya tiba vya kuwahudumia watoto
mara wapougua na kufikishwa kwenye hospitali hiyo.
Vifaa hivyo vina thamani ya Dola
za Kimarekani Laki moja sawa na zaidi Sh milioni 2 vimetolewa na
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF),kwa lengo la
kupunguza vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
Baadhi ya vifaa vilivyotolewa
ni Ventilator, medical, adult –child ,w/access pamoja na Warmer system ,
newborn, radiant, w/access.
Akizungumza wakati wa kukabidhi
vifaa hivyo Mwakilishi wa UNICEF Tanzania Dk Jama Gulaid amesema
mchango wa UNICEF na michango ya wadau wengine itawezesha watumishi wa
hospitali ya Muhimbili kuokoa maisha ya watoto ambao wanahitaji huduma
za afya.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando amesema hadi
kufikia mwaka 2013 Tanzania imefanikiwa kupunguza vifo vya watoto hao
kwa theluthi mbili.
Kwa mujibu wa Dk Mmbando, mwaka
2013 Tanzania imepunguza vifo hivyo na kufikia 54 kwa vizazi hai 1,000
na kufikia lengo la Milenia na kwamba mafanikio hayo yametokana na
kiwango kikubwa cha chanjo , matumizi sahihi ya dawa za Malaria pamoja
na vyandarua.
Kwa upande wake Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Mseru amewashukuru UNICEF
kwa msaada huo ambao utachangia kwa kiasi kikubwa kuokoa maisha ya
watoto na kuboresha huduma za afya .
Comments
Post a Comment