KAMATI YA STARS, YAWASHUKURU WATANZANIA
Mwenyekiti
wa Kamati Taifa Stars, Farouqh Baghozah amewashukuru watanzania kwa
michango yao waliyoitoa kuispaoti timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ katika
michezo ya kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi dhidi ya
Algeria.
Farouqh alianza kwa kuwashukuru watanzania kwa kujitokeza kwa wingi katika mechi ya Taifa Stars na Algeria na kuwashukuru pia wale wote waliosafiri na timu hiyo ya Taifa, Taifa Stars kwenda Algeria katika mechi ya marudiano.
Pia Mwenyekiti amechukua fursa
hiyo kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Makamu wa
Raisi Mama Samiha Suluhu, Raisi Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mkuu wa Mkoa wa
Dar Es Salaam na Pwani na viongozi wote wa chama na serikali kwa njia
moja au nyingine katika kusapoti timu ya Taifa Taifa Stars kwenye Mchezo
na Algeria
Naye Mkuu wa mkoa Dar es salaa,
ambaye ni mlezi wa kamati hiyo, Mh Mecky Sadick aliwashukuru watu wote,
kuanzia wanakamati kwa jinsi walivyojitoa kwa muda wao wote katika
maandalizi na hasa kuhamasisha watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani
kuishangilia timu yao ya taifa kwa kuomnyesha uzalendo.
Kwa namna ya kipekee Mecky Sadick
amewashukuru watu wote na makampuni yaliyojitokeza katika kuchangia Timu
ya taifa wakiwemo Jubilee Insurance, Equity Bank, PPF, Serena Hotel,
GSM, bila kusahau vyombo vote vya habari ambavyo kwa namna moja au
nyingine waliweza kujitoa na kuhamasisha watanzania wajitokeze kwa wingi
uwanja wa taifa kuishangilia timu yao.
Katika mchakato mzima wa awali wa
mechi ya kufuzu kombe la dunia 2018, Kamati kupitia kwa wadau mbalimbali
iliweza kuchangisha pesa jumla ya milioni 122,640,000 za kitanzania,
dola za kimarekani 19,800 na 177,000 kutoka tigo pesa na airtel money.
Matumizi ni dola za kimarekani 70355, na milioni 47,904, 743 za kitanzania.
Mwisho kamati imewashukuru sana Watanzania na na kuwaomba wadumishe umoja wtue.. Nchi Yangu, Timu Yangu Taifa langu.
Comments
Post a Comment