ALIKIBA AKANUSHA TETESI ZA KUMPA UJAUZITO JOKATE
Baada ya tetesi kuzagaa kwenye baadhi ya vyombo vya bahari na
mitandao ya kijamii kuwa mrembo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, kuwa ni
mjamzito na mhusika mkuu wa ujauzito huo ni mwanamuziki Ali Kiba,
mwanamuziki huyo akanusha madai hayo.
Katika moja ya gazeti pendwa la udaku liliandika kuwa wakati mwanadada Wema Sepetu, akihaha kutafuta mtoto ili kuwa na familia, mwanamitindo Jokate, amenasa ujauzito ambapo mhusika mkuu ni Ali Kiba.
Inadaiwa kuwa kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Jokate, alidai kuwa Jokate, ana kila dalili ya kuwa mjamzito kwa kuwa amekuwa mtu wa kupenda embe mbichi na kusumbuliwa na tumbo mara kwa mara.
Mtu huyo hakuishia hapo na kudai kuwa mimba hiyo ina miezi miwili na kudai kuwa wazazi wa mrembo huyo wamekuwa wakali kama mbogo baada ya kusoma habari ya ujauzito wa binti yao kwenye gazeti kabla ya ndoa.
Kwa mujibu wa Ali Kiba, amedai kuwa hawezi kuanika uhusiano wake na kudai kuwa sio kweli hizo tetesi na wala hatarajii kupata mtoto na mrembo Jokate.
Hayo ameyasema baada ya kugusiwa swali la tetesi za ujauzito wa mwanamitindo huyo alipoalikwa na mwanamuziki mwenzake Christian Bella, katika kipindi kimoja redioni.

Comments
Post a Comment